Moyo Media - Adz

Moyo Media - Adz

Friday, September 2, 2011

HISTORIA : Y2K

Katika ulimwengu wa teknohama kuna matatizo mengi ambayo hupelekea kuwepo kwa upotevu na uharibifu wa taarifa . Unapozungumzia suala hili unaweza fikiria ni masihara .
Mnamo mwaka 2000 kulitokea tukio la kihistoria katika ulimwengu wa teknohama duniani . Tukio hilo lilijulikana kama Y2K ( Y - Year . K - SI Unit PREFIX KILO  = 1000 . 2K = 2000 ) .
Ni tukio ambalo halikujarajiwa na wataalamu wa mifumo ya kompyuta walishindwa kugundua tatizo hili kwamba linaweza kutokea , kwa sababu katika maandalizi ya mifumo kompyuta hiyo ikiwasilishwa kwa tarakimu mbili tu za mwaka kwa mfano 1980 iliwasilishwa kama 80 .
Ilipofikia January 1 , 2000 , mifumo ya kompyuta ilishindwa kutofautisha kati ya 2000 au 1900 . Baadhi ya mifumo zilijaribu kuitambulisha mwaka 2000 kama 19100 .
Tatizo hili lilisababisha kompyuta kotofanya kazi ipaswavyo kutokana na mifumo kutobagua mwaka gani uliopo .
Hatimae iliathiri uchumi wa mataifa , makampuni , sekta mbali mbali ulimwenguni ,zikiwemo sekta za afya , fedha , bima , usalama n.k

No comments: